Connect with us

Makala

Metacha Langoni Kuikabili Tp Mazembe

Kipa wa klabu ya Yanga sc Metacha Mnata atasimama langoni katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kati ya klabu yake na Tp Mazembe utakaofanyika nchini Congo Drc mapema mwezi ujao.

Metacha analazimika kukaa langoni baada ya kipa namba moja wa klabu hiyo Djigui Diara kuwa na kadi mbili za njano hivyo kwa mujibu wa sheria na kanuni za mashidano hayo staa huyo atakosa mchezo mmoja na hatimaye kadi hizo kufutika na kuwa huru kucheza michezo inayofuatia ya robo fainali.

Diara alipata kadi ya kwanza katika hatua ya mtoani dhidi ya Club Africain uliofanyika nchini Tunisia na juzi alipata kadi ya njano katika mchezo dhidi ya Us Monastr uliofanyika nchini na Yanga sc kupata ushindi wa mabao 2-0 yaliyoiwezesha klabu hiyo kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Mbali na Diara wengine watakaoukosa mchezo huo ni Djuma Shabani huku presha kubwa ipo kwa Kennedy Musonda, Stephane Aziz Ki, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya ambao wana kadi moja za njano hivyo wakipata nyingine wataukosa mchezo ijayo ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala