Mbeya City Atupia Mabao 2-1 Leo

0

Mbeya City imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa leo Octoba 23,wa ligi kuu bara uliochezwa uwanja wa Kaitaba.

Kwa mara ya kwanza Mbeya City leo wanasepa na pointi tatu kwa msimu wa 2020/21 tangu kuanza wa ligi ikiwa ni raundi ya nane.

Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Abdurazack Mohamed  kwa mkwaju wa penalti dakika ya pili huku lile la pili lilifungwa dakika ya 24 na Siraj Juma.

Bao la kufutia machozi la Kagera Sugar lilipachikwa kupitia Erick Kyaruzi dakika ya 46.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kutoka nafasi ya 18 iliyokuwa kwa muda wa raundi saba na sasa ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi nane ndani ya ligi huku Kagera Sugar inabaki nafasi ya 15 ikiwa imecheza mechi nane na pointi tano zikiwa zimetofautiana kwenye mabao ya kufungwa na kufungana.

Leave A Reply

Your email address will not be published.