Connect with us

Makala

Mayele Azua Tafrani

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Fiston Kalala Mayele amezua tafrani katika mitandao ya kijamii baada ya taarifa kusambaa kuwa amejiunga na klabu ya Kaizer Chiefs kwa mkataba wa miaka miwili inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika ya Kusini.

Taarifa zilianza kutolewa na mwandishi maarufu Afrika magharibi Nuhu Adam ambapo alitoa taarifa hiyo iliyowashtua wadau wa michezo nchini kiasi cha Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga sc kuthibitisha kupokea ofa kutoka klabu hiyo pamoja na RS Berkane ya Morroco lakini msimamo wa klabu hiyo ni kutomuuza mchezaji huyo ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja klabuni hapo.

“Mayele haondoki Yanga sc na kama akiondoka na mimi Ninaondoka”Alisema Afisa Mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga sc Senzo Mazingiza wakati akiongea na moja ya redio maarufu za michezo hapa nchini.

Hata hivyo licha ya habari hiyo taarifa za kuthibitisha ni kwamba mchezaji huyo ana mkataba wa mwaka mmoja uliosalia klabuni hapo hivyo ni ngumu kuondoka huku klabu ikiwa haina mpango wa kumuuza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala