Connect with us

Makala

Manyika Kufanya Maajabu Polisi

Golikipa aliyewahi kuichezea Simba Sc na Singida United Peter Manyika ameaminika mbele ya uongozi wa Polisi Tanzania kuwa atafanya vizuri katika mechi za ligi kuu bara na mashindano ya kombe la FA.

Polisi Tanzania inayomilikiwa na jeshi la polisi nchini ilimsajili Manyika katika usajili wa dirisha dogo mwezi huu akitokea katika klabu ya KCB inayoshiriki ligi kuu Kenya.

Munisi alisema kuwa wanaamini kuwa Manyika ni mmoja wa watakaowavusha katika msimu huu ili kufikia nafasi ya tatu za juu na waweze kucheza fainali za kombe  la FA linalotoa tiketi za kuwakilisha Tanzania Bara kushiriki kombe la shirikisho Afrika.

Polisi Tanzania ipo nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi kuu bara ikiwa imecheza mechi 16 na pointi 24 wakati mabingwa watetezi Simba Sc ina pointi 41 na inaongoza katika msimamo wa ligi kuu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala