Connect with us

Makala

Man Utd Gari Limewaka

Tambo za mashabiki wa klabu ya Manchester United zimekua nyingi hasa baada ya timu hiyo kufanikiwa kuisambaratisha Manchester City kwa mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford na kufanikiwa kuingia rasmi katika mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini humo msimu huu.

City ikiwa chini ya mkufunzi Pep Guardiola ilifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo likifungwa na Jack Grealish kwa kichwa lakini Bruno Fernandes alifunga bao la utata dakika ya 78 akisawazisha huku wengi wakizani kuwa bao hilo ni Offside ambapo kabla ya kufunga Marcus Rashford aliingilia mchezo akiwa ameotea lakini mwamuzi alitafsiri sheria na kuamua kuwa ni bao halali.

Dakika nne baadae Marcus Rashford aliipatia United goli la ushindi akiunganisha krosi kinda ya Alejandro Garnacho ambapo mpaka dakika tisini za mchezo zinamalizika united ilipata alama tatu nakufikisha alama 38 katika nne bora ya msimamo wa ligi.

Manchester United chini ya Eric Ten Hag imekua na matokeo ya kufurahisha ikiwa imeshinda mechi 12 kati ya 13  katika mashindano yote msimu huu huku ikishinda michezo 9 mfululizo na kurejea katika mbio za ubingwa baada ya kuanza msimu vibaya.

Ushindi huo mfululizo kwa Manchester Unted umechagizwa pia na kiwango bora cha Marcus Rashford ambaye amefunga katika michezo saba mfululizo tangu alivyofanya Cristiano Ronaldo mwaka 2008 huku pia nidhamu yake ikiwa imeboreka vya kutosha tangu apewe adhabu ya kukosa mchezo mmoja na kocha Eric Ten Hag baada ya kulala na kuchelewa mazoezini.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala