Connect with us

Makala

Makocha Yanga sc,Simba sc Wafunguka Derby

Kuelekea mchezo wa ngao ya jamii baina ya Yanga sc na Simba sc utakaofanyika kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam makocha wa timu zote mbili Zoran Maki na Mohamed Nabi wamefunguka kuhusu mchezo huo ambao utakua ndio mchezo wa kufungua pazia la ligi kuu nchini.

Katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika hivi punde katika makao makuu ya shirikisho la soka nchini (Tff) yaliyopo Karume makocha hao pamoja na manahodha John Boko na Bakari Mwamnyeto walipata wasaa wa kuzungumza machache.

“Nimecheza derby kubwa kama Morocco,Sudan,Algeriana na hata Saudi Arabia hivyo hata ya kesho haitakuwa tofauti, lakini cha muhimu kwetu ni kupata Ushindi”
“Mchezo wa kesho ni derby hakuna kitu kikubwa cha tofauti. Wachezaji wanatakiwa kujua ni ngumu lakini tumejiandaa kufanya vizuri” Alisema  Zoran Maki kocha wa Simba.
“Najivunia kuwa kocha niliyecheza mechi nyingi za Derby hapa Tanzania, tumefanya maandalizi lakini Derby imekuja muda mfupi baada ya kumaliza ligi lakini tutahakikisha tunapambana na hatimaye ushindi utakuwa wetu.Alisema kocha ya klabu ya Yanga sc Nasredine Nabi
” sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri hakuna mwenye majeraha zaidi ya Kambole lkn naye anaendelea vizuri na hata Msimu uliopita pia tulipoteza (vs Zanaco) lakini tukabeba kombe hata sasa kisaikolojia bado tuko vizuri licha ya kupoteza mchezo wa kirafiki (vs Vipers) “.
” Hatuna presha yoyote, njooni mashabiki ikiwepo suprise mtaipata hapo hapo uwanjani, ninyi mfike kushangilia”Alisema nahodha wa klabu ya Yanga sc Bakari Nondo Mwamnyeto
Msimu uliopita klabu hizo zilikutana katika mchezo wa ngao ya jamii kama huu wa kesho na Yanga sc ilishinda kwa 1-0 bao likifungwa na Fiston Kalala Mayele.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala