Connect with us

Makala

Maki,Akpan Kimeeleweka Simba sc

Kikao baina ya kocha Zoran Maki na uongozi wa juu wa klabu hiyo pamoja na mchezaji Victor Akpan kimezaa matunda baada ya kukubaliana kuwa mchezaji huyo asalie kikosini badala ya kuachwa ama kutolewa kwa mkopo licha ya kusajiliwa hivi karibuni akitokea klabu ya Coastal Union.

Mchezaji huyo ambaye alishiriki kambi ya maandalizi ya msimu mpya ya klabu hiyo nchini Misri inadaiwa kuwa kocha Zoran Maki hakuridhishwa na uwezo wa kiungo huyo hivyo kuamuru asajiliwe kiungo mwingine kuziba nafasai yake.

Changamoto kubwa iliyosababisha Akpan kusalia klabuni hapo kwanza ni mshahara anaolipwa klabuni hapo shilingi Milioni sita imekua shida kwa baadhi ya klabu za ligi kuu kuweza kumlipa hivyo kukosa timu ya kuichezea kwa mkopo huku pia imekua ngumu kumtema kutokana na kuwa na mkataba mpya kabisa wa miaka miwili na pia imekua ngumu kusajili kiungo mwingine wa kigeni mpaka wamuache mchezaji mmoja baada ya kuwa tayari wametimiza idadi ya wachezaji 12 kwa mujibu wa kanuni.

Zoran Maki amekubali kuendelea na kiungo huyo huku akijiandaa kumpa mazoezi maalumu ili kumbadilisha aendane na majukumu na mfumo ambao kocha huyo anautaka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala