Connect with us

Makala

Liverpool Waipa Kichapo Wolves Cha Mabao 2-1

Timu inayoongoza kwenye ligi kuu England ikiwa nafasi  ya kwanza Liverpool imewapa kichapo cha mabao 2-1 timu ya Wolves katika mchezo wa jana uwanja wa Molineux Stadium chini ya refa kutoka England Michael Oliver.

Liverpool walianza kupata bao la kwanza dakika ya 8 kupitia Jordan Henderson huku bao la kusawazisha kutokea Wolves lilipatikana kupitia Raul Jimenez dakika ya 51.

Dakika ya 56 Andy Robertson kutokea Liverpool alipokea kadi ya njano na baadaye Roberto Firmino aliongeza furaha ya mashabiki dakika ya 84 kwa kufunga bao la pili.

Wolves inakuwa nafasi yya 7 katika msimamo wa ligi kuu England ikiwa imecheza mechi 24 na pointi 34 huku Liverpool inabaki kuongoza na pointi 67 ikiwa imecheza mechi 23.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala