Liverpool Vs Arsenal Kukiwasha Kesho

0

Premier League msimu huu umeanza vizuri sana baada ya wikiendi iliyopita kuwepo na mtanange wa kukata na shoka,huku jumatatu ya kesho Liverpool watawakaribisha maasimu wao Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani Anfield ili kuendelea kunogesha EPL saa 4 usiku.

Mchezo huo wa kesho unakuwa ni wa burudani sana kwa mashabiki kesho kwani si mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana msimu huu,kwani tayari Arsenal walishawaburuza Liverpool katika mchezo wa ngao wa jamii.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England wanasubiri kwa hamu kuona kama Arsenal watarudia walichokifanya siku ya ngao ya jamii kwani mechi itakuwa ni ya kisasi ili kila mmoja aweze kuzipata pointi tatu muhimu.

Leave A Reply

Your email address will not be published.