Ligi ya mabingwa inaendelea leo ambapo watetezi wa ligi kuu England,Liverpool itavaana na Ajax majira ya saa 4:00 usiku uwanja wa Johan Cruijff Arena.
Huu ni mchezo wa aina yake katika ulimwengu wa soka ambapo unatukumbusha mwaka 1966 walipokutana na hawajawahi kukutana tena mpaka sasa.
Ajax ni miamba ya soka nchini Uholanzi na leo Oktoba 21,watawakaribisha miamba ya soka la Uingereza,Liverpool.
Liverpool inakwenda kukutana na Ajax kwenye mchezo huu bila mlinzi wao hodari Virgil Van Dijik na golikipa wa Alisson Becker, japo bado wanaonekana kuwa tishio kwa Ajax kwani hawajawahi kuifunga Liverpool mara mbili tangu walipokutana.