Ligi Kuu Kuendelea Leo Tanga

0

Ligi kuu bara inaendelea leo ambapo raundi ya nne inakamilika kwa mechi moja kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani majira ya saa 10:00 jioni kati ya Coastal Union inayonolewa na Juma Mgunda dhidi ya JKT Tanzania inayonolewa na Mohamed Abdalah.

Coastal Union imetoka kulazimisha sare ya bila kufungana mchezo wake uliopita mbele ya Dodoma Jiji huku JKT Tanzania inaingia uwanjani kupambana na Coastal Union ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania.

Timu zote zimejipanga vyema katika mchuano wa leo ikiwa wote wanaziataka pointi tatu muhimu.

Leave A Reply

Your email address will not be published.