Connect with us

Makala

Letaaa Mzunguuuu

Mzungu wa klabu ya Simba sc Dejan Georgijević amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza kwenye ligi kuu msimu huu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na kuipa alama tatu klabu yake katika ushindi wa mabao 2-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Simba sc iliandika bao la kwanza dakika ya 42 kupitia kwa Moses Phiri aliyeunganisha kwa kichwa mpira uliogonga mwamba wa Cletous Chama ambaye alipiga faulo kali iliyomshinda golikipa wa timu ya Kagera Sugar.

Kipindi cha pili kocha Zoran Maki alimwingiza Dejan Georgijević kucheza kama mshambuliaji wa kati hivyo kupelekea kupata bao la pili dakika ya 81 ya mchezo akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Kagera Sugar ambaye alijichanganya wakagongana na beki wake.

Mashabiki wa klabu ya Simba sc waliimba jina la mzungu huyo baada ya dakika 90 za mchezo huku Simba sc ikikaa kileleni mwa msimamo na alama 6 na mabao matano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala