Taarifa kutoka nchini Ubelgiji zinadai kuwa staa wa klabu ya Coastal Union Lameck Lawi yuko mbioni kurejea nchini baada ya kufeli majaribio katika klabu ya K.A.A Gent inayoshiriki ligi kuu nchini humo.
Awali Taarifa zilisema kuwa Lawi ambaye aligomewa kujiunga na Simba sc na Uongozi wa klabu hiyo kwa kuwa anadili nchini humo la kusajiliwa moja kwa moja lakini alipofika alianza mazoezi na timu hiyo ili kumtazama zaidi uwezo wake.
Ambapo sasa klabu hiyo imeonekana kutoridhishwa na uwezo wake hivyo usajili huo unaweza kukwama na mabosi wa klabu hiyo ya Coastal Union sasa wanahaha kumtafutia timu nyingine nchini humo ama barani Ulaya.
Huku hayo yakiendelea kwa upande wa nyumbani klabu hizo ziliambiwa zikae chini na kamati ya Usajili na hadhi za wachezaji ili kutatua mgogoro baina ya pande hizo za Simba sc na Coastal Union ili kumaliza suala hilo kiungwana ambapo licha ya Coastal Union kurudisha pesa za usajili wa beki huyo kwa Simba sc bado mchezaji huyo anadaiwa pesa za kusainia mkataba ambazo alilipwa katika akaunti yake moja kwa moja na hajazirudisha mpaka sasa.
Ombi la Coastal Union kwa Simba sc ni kuwa itawalipa pesa hizo na faida juu ikiwa itakamilisha uuzaji wa beki huyo kwa bei ya juu zaidi barani Ulaya ambako mpaka sasa dili hilo limekua gumu kufanyika na Simba sc wakikomaa kuwa wao ndio wanapaswa kumuuza mchezaji huyo kwa kuwa ni mali yao.