Kocha Azam Fc Akalia Kuti Kavu

0

Kocha wa klabu ya Azam Fc Arstica Cioaba amekalia kuti kavu katika klabu hiyo baada ya kuwa na msululu wa matokeo mabovu klabuni hapo.

Kocha huyo Mromania jana alishindwa kuiweka Azam Fc kileleni baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Yanga sc huku akitoka kufungwa wikiendi iliyoisha na Kmc.

Kocha huyo amepata ushindi mara moja kati ya mechi tano huku akitoka sare mara moja na kupoteza mechi tatu na kuisababishia klabu hiyo kupata alama 4 katika ya 15.

Mpaka sasa taarifa za ndani zinadai kocha huyo anaweza kutimuliwa muda wowote kuifundisha klabu hiyo kutokana na matokeo hayo.

Leave A Reply

Your email address will not be published.