KMKM Vs Yanga Kitaeleweka Leo

0
KMKM Sc ya Zanzibar tayari imewasili leo jijini Dar tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga Sc utakaochezwa leo Septemba 30,uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.

 

Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku ukiwa na malengo ya kukiweka sawa kikosi cha Yanga kwa ajili ya mechi ijayo ya ligi kuu bara dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Octoba 3,uwanja wa Mkapa.

 

Mechi ya leo kati ya Yanga inayonolewa na kocha mkuu ,Zlatko Krmpotic didi ya KMKM kiingilio ni 5,000 kwa mzunguko huku VIP ni 10,000.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.