Home Makala Kmc Yatawala Tuzo Septemba

Kmc Yatawala Tuzo Septemba

by Sports Leo
0 comments

Kocha AbdulHamid Moallin pamoja na mchezaji Waziri Junior wamefanikiwa kuchukua tuzo za kocha bora na mchezaji bora wa mwezi septemba kutoka na taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi kuu nchini.

Waziri amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo  akiwashinda Jean Baleke wa Simba na John Nakibinge wa Tabora United alioingia nao fainali.

Moalin amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo akiwazidi Roberto Oliveira wa Simba na Abdallah Mohamed wa Mashujaa FC baada ya kufanikiwa kuiongoza Kmc kuibuka na alama katika michezo yote iliyochezwa katika mwezi Septemba.

banner

Pia kamati ya tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Amir Juma kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Septemba kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu, uwanjani hapo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited