Connect with us

Makala

Kmc Vs Tanzania Prisons Kesho Uhuru

Kikosi cha KMC FC kimekamilisha maandalizi kuelekea katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi Tanzania Prisons ikiwa ni mara baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kalenda ya Shirikisho la soka Duniani (FIFA).

KMC FC kesho itawakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam mchezo ambao utapigwa saa 16:00 jioni na kwamba wachezaji wote wapo tayari kwa mtanange huo.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu Thierry Hitimana imekuwa na wakati mzuri wakufanya maandalizi tangu ilipocheza mchezo wa mwisho Mei 19 dhidi ya Mbeya City na kuondoka na ushindi wa magoli matatu kwa bila.

Katika kipindi chote ambacho Timu zilikuwa kwenye mapumziko, KMC iliingia kambini Mei 27 na kuanza program mbalimbali ambapo zimefanyika kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kucheza mechi za kirafiki na kwamba hadi sasa Ligi inarejea kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo huo licha ya kwamba utakuwa na ushindani kutokana na kila Timu kuhitaji matokeo.

“Tunakwenda kwenye mechi ngumu na bora, tunafahamu Prisons ni wazuri wanajipanga wasipoteze, lakini kwa upande wa KMC tunajua ubora wa wachezaji wetu tulionao pamoja na benchi la ufundi hivyo tunahitaji kutumia vizuri uwanja wetu wa nyumbani kuzipata alama tatu.

“Ligi hivi sasa inakwenda ukingoni na kila mtu anahitaji kutetea nafasi ya kuendelea kuwepo katika msimu ujao, ndio mana tunafahamu ugumu wa mchezo wa kesho, lakini mashabiki wasihofu, timu imeandaliwa vizuri na kwamba wajitokeze kutoa sapoti ili kuongeza morali zaidi kwa wachezaji.

Imetolewa leo Juni 13
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano KMC FC

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala