Connect with us

Makala

Kichuya Kurejea Simba sc

Taarifa zinasema Uongozi wa Klabu ya Simba upo kwenye mazungumzo ya kutaka kumrejesha kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya katika kikosi cha Wekundu hao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi 2022/23.

Tayari mazungumzo ya kumrejesha Kichuya mpaka sasa yamefikia pazuri mabapo atasaini mkataba wa miaka miwili baada ya kuwa huru akiwa amemaliza mkataba wake katika klabu ya Namungo Fc yenye makao yake mkoani Mtwara ambapo alijunga akitokea klabu ya Pharco Fc ya nchini Misri.

Kichuya amekua na msimu mzuri katika klabu ya Namungo Fc msimu huu akiwa amechangia upatikanaji wa mabao nane akifunga matano na kusaidia upatikanaji wa mabao matatu katika ligi kuu msimu huu.

Simba sc awali iliwahi kumsajili Kichuya akitokea Mtibwa Sugar ambapo baada ya kucheza kwa misimu kadhaa klabuni hapo alikwenda nchini Misri katika klabu ya Pharco Fc ambayo ilimpeleka katika klabu ya Enppi alikocheza kwa mkopo kisha akarejea Simba sc na baadae kujiunga Namungo Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala