Kaze Kufungua Dimba Na Polisi Tanzania

0

Cedric Kaze ambaye ni kocha mkuu wa Yanga Sc tayari ameshaanza kazi ya kukinoa kikosi hicho cha Jangwani ambacho Novemba 22,kitavaana na Polisi Tanzania uwanja wa Mkapa.

Kocha huyo aliyesaini kandarasi ya miaka miwili kukipa makali kikosi cha Yanga Sc atakutana na Polisi Tanzania ambayo iko nafasi ya 7 na pointi 10 ikiwa imecheza mechi tano huku kikosi chake kikiwa nafasi ya tatu na pointi 13.

Mchezo huo wa raundi ya sita wa ligi kuu unatarajiwa kuchezwa majira ya 1:00 usiku ambapo kutakuwa na ushindani mkubwa kwani kila timu itakuwa ikisaka pointi tatu muhimu.

Leave A Reply

Your email address will not be published.