Juventus Yakomaa Na Dybala

0

Tarifa zinaeleza kuwa Juventus ina mpango wa kumpatia mkataba mpya Paulo Dybala kwani ni mchezaji bora na tegemeo ndani ya timu hiyo.

Dybala anakaribia kumaliza mkataba wake ndani ya Juventus mwezi Juni 2022 ,hivyo mabosi hao wanapanga kumuongezea mkataba wa miaka mitano ambapo atakuwa analipwa euro milioni 10 kama bonasi na kuwa mchezaji wa pili kulipwa vizuri ndani ya kikosi hicho baada ya Cristiano Ronaldo.

Msimu uliopita Dybala aliibuka kuwa mchezaji bora ndani ya serie A, huku akiisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kuifikisha hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya.

Leave A Reply

Your email address will not be published.