Jacob Mulee Kocha Mpya Kenya

0

Jacob Mulee ametangazwa jana Octoba 21 na Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Kenya (FKF),Nick Mwendwa kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya Hrambee Stars.

Mulee mwenye umri wa miaka 52 amesaini kandarasi ya miaka mitatu akipokea mikoba ya Francis Kimanzi aliyeachana na miamba hao wa soka siku mbili zilizopita akiwa pamoja na benchi la ufundi.

Benchi la ufundi lililoondoka na Francis ndilo lililoiwezesha Kenya kufuzu kucheza AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya ya miaka 15.

Mwendwa ana matumaini makubwa kwa Jacob kwani ni kocha anayeujua mpira wa Kenya na amekuwa hapo akiucheza,ameshinda ligi ameshinda mataji mbalimbali ikiwemo Cecafa na amekuwepo pia kwenye michuano ya AFCON hivyo anaamini watapiga hatua kubwa msimu huu wa 2020/2021 katika ligi kuu Kenya.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.