Hoffenheim Waipa 4G Bayern Munich

0

Bayern Munich imenyooshwa kwa kuchapwa mabao 4-1 mbele ya Hoffenheim kwenye mchezo wa Bundesliga uliochezwa jana kwenye uwanja wa Rhein-Neckar.

Mabao ya Hoffenheim yalipachikwa na Ermin Bicakcic dakika 16, Mu’nas Dabbur dakika ya 24 na Andrej Kramaric alipachika mabao mawili dakika ya 77 na 90+2 kwa mkwaju wa penalti.

Munich walipachika bao kupitia Joshua Kimmich dakika ya 36 huku wakiondoka baada ya dakika 90 kukamilika wakiwa kama wamemwagiwa maji.

Mara ya mwisho Bayern Munich kupoteza mchezo ndani ya dakika 90 ilikuwa ni Januari 11 mwaka huu ambapo ilichapwa mabao 5-2 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Numberg.

Leave A Reply

Your email address will not be published.