Connect with us

Makala

Hapatoshi Yanga sc Vs Coastal Union

Kesho ndio siku ya kulipiza kisasi ndivyo wanavyosema mashabiki wa klabu ya Coastal union baada ya kufungwa katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho na klabu ya Yanga sc mwishoni mwa msimu ulioisha licha ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 3-3 na Coastal kupoteza kwa matuta.

Timu hizo zitamenyana kesho katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu nchini utakaofanyika katikam uwanja ule ule wa fainali wa Sheikh Amri Abeid Kaluta jijini Arusha ambapo Coastal union atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

Vikosi vya timu zote mbili vina mabadiliko kadhaa ambapo kuna wachezaji wameondoka na wengine wamekuja hasa upande wa Coastal union ambapo Abdul Sopu, Paschal Kitenge na Amani Peter pamoja na Victor Akpan ni mastaa ambao hawatakuwepo hapo kesho huku Yanga sc ikiwa na muongezeko wa Benard Morrison na Aziz Ki katika eneo la ushambuliaji.

Timu zote mbili zimeibuka na ushindi katika raundi ya kwanza ambapo Yanga sc imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union wakiichapa Kmc 1-0 katika uwanja huo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala