Connect with us

Makala

Gsm Wajitoa Udhamini Ligi Kuu

GSM imejiondoa Rasmi kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Tanzania bara kutokana na kutotimizwa Kwa Makubaliano ya Mkataba baina yao na Shirikisho la soka nchini (TFF).

Kampuni hiyo ambao ni wadhamini wenza wa Ligi Kuu Bara wametangaza kujitoa kudhamini ligi hiyo leo Februari 7 ikiwa ni siku 76 tangu wasaini mkataba wa Sh2.1 bilioni Novemba 23.

Gsm katika mkutano wake na waandishi wa habari nchini wametangaza kujitoa kutokana na bodi ya ligi kuu nchini (TPLB) pamoja na Tff kushindwa kukamilisha masharti ya kimkataba ambao waliingia na kampunin hiyo ikiwemo klabun zote kuvaa nembo ya kampuni hiyo mabegani.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa GSM Ghalib Mohamed amejiuzuru kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ushindi ya Taifa Stars.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala