Gabon Wafanyiwa Figusu

0

Pichani inayosambaa ikiwaonyesha  Wachezaji wa timu ya taifa ya Gabon walivyolala usiku kwenye Uwanja wa Ndege huko Gambia, saa chache kabla ya mchezo wao wa leo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kwa mujibu wa nahodha wa Gabon Aubameyang amesema serikali ya Gambia imewashikilia na kuwapokonya passport zao bila sababu zozote za msingi na kuwatelekeza uwanjani hapo ikidai hawaruhusiwa kwenda hotelini kwa kuwa hawajapima virusi vya Corona.

Hata hivyo taarifa zinadai  Hii inaonekana ilifanywa kulipiza kisasi kwa kile Gambia ilichokitaja kama matibabu sawa na kile walichofanyiwa huko Libreville walipokwenda kwa ajili ya mchezo wa awali.

Leave A Reply

Your email address will not be published.