Connect with us

Makala

Fei Toto Aigomea Yanga sc

Baada ya Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuamua kuwa mchezaji Feisal Salum anapaswa kurudi katika klabu ya Yanga sc kutokana na kutofuata taratibu katika kuvunja mkataba wake,Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine amemuandikia barua mchezaji huyo ya kurejea kambini.

Licha ya kupokea barua hiyo mchezaji huyo amegoma kurejea katika kambi ya klabu hiyo iliyoko Kigamboni eneo la Avic Town ambapo ameendelea na mazoezi binafsi akijiweka fiti huku pia akiomba rejeo katika kesi hiyo ambayo iliwapa Yanga sc ushindi.

Feisal katika kuomba marejeo ya hukumu hiyo ameongeza idadi ya mawakili ili kuhakikisha kuwa anashinda kesi hiyo ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Yanga sc ambapo hukumu ya awali ya kamati hiyom ilimsisitiza kuwa mchezaji huyo ni mali ya Yanga sc na hivyo kutakiwa kurejea klabuni hapo.

Feisal aliibuka kuwa kipenzi cha mashabiki wa Yanga sc tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea Jku ambapo awali alisaini Singida United lakini makubaliano kati ya Yanga sc na Singida United yalimshuhudia staa huyo akitua Yanga sc ambapo amecheza kwa kiwango kikubwa sana.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala