Connect with us

Makala

Farid Ajifunga Miwili Yanga sc

Kiungo Farid Musa Malick amesaini  mkataba wa miaka miwili kuendelea kusalia katika klabu ya Yanga sc mpaka mwaka 2024baada ya ule wa awali kuelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Farid ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari kuwa amesaini mkataba huo akiwa chini ya meneja wake mpya Oscar Oscar na kuzima maswali ya wadau wa soka ambao walikua wakijiuliza kama bado ana ndoto za kusaka timu nje ya nchi.

Awali wakati anajiunga na klabu hiyo miaka miwili iliyopita staa huyo alinukuliwa akisema kwamba ana mpango wa kwenda nje ya nchi kucheza soka lakini atasalia nchini kwa muda kutokana na Janga la Corona lililosababisha akose timu ulaya na hivyo akaamua kujiunga na Yanga sc.

Hata hivyo Farid ndani ya kikosi cha Yanga sc amefanikiwa kumvutia kocha Nasredine Nabi ambaye amekua akimtumia kama kiraka katika nafasi za beki wa pembeni,kiungo na winga hivyo kuongezewa mkataba wa kusalia jangwani lilikua ni jambo lililotarajiwa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala