Connect with us

Makala

Djuma,Diarra Hatihati Kuwavaa Azam Fc

Kocha wa Klabu ya Yanga sc Nasreddine Mohamed Nabi amesema kuwa wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza Djuma Shabani na Djigui Diarra wana hatihati ya kuwavaa Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu nchini siku ya kesho kutokana na sababu mbalimbali za kiafya.

Nabi alisema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari unaoandaliwa na bodi ya ligi kuu ambapo makocha huongea na waandishi wa habari za michezo siku moja kuelekea katika mchezo huo ambapo amesema kuwa Djuma alikua na Maralia siku chache zilizopita lakini ameanza mazoezi huku Diarra alikua na majeraha japo naye ameanza mazoezi hivyo kuwatumia inategemea na ripoti ya daktari.

Yanga sc na Azam Fc zitamenyana kesho katika uwanja wa Azam Complex Chamazi ambapo mara ya mwisho Yanga sc ilishinda kwa mabao 2-1 na kuondoka na alama zote tatu muhimu.

Kocha wa Azam Fc Kali Ongala alisema kuwa wanajua Yanga sc iliwafunga msimu uliopita lakini sio timu hatari hivyo watajitahidi kuwatuliza mashabiki ili wapate alama tatu muhimu kwani mashabiki wa Yanga sc wamekua wanaongeza hamasa kwa wachezaji wao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala