Connect with us

Makala

Cas Yapokea Barua ya Yanga sc

Mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo duniani (CAS) imethibitisha rasmi kuwa imepokea barua rasmi kutoka klabu ya Yanga Sc juu ya malalamiko yao kwa TFF, Bodi ya Ligi na Klabu ya Simba Sc juu ya sakata lao la kariakoo Dabi.

Yanga sc iliwasilisha malalamiko Cas ikipinga kitendo cha bodi ya ligi kutowapa alama tatu baada ya kuahirisha mchezo baina yake na klabu ya Simba Sc uliokua ufanyike machi 8 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo Yanga sc inasisitiza kupewa alama tatu kutokana na klabu ya Simba Sc kuvunja kanuni kwa kuamua kugomea mchezo huo kwa sababu ya kuzuiwa kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi.

Katika kesi hiyo walalamikiwa ni Shirikisho la soka nchini (TFF),bodi ya Ligi na Simba Sc ambao  wamepewa siku 10 baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka CAS kuanza kuandaa utetezi wao wakati mchakato wa kesi unaanza kusikilizwa rasmi na kwa haraka.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 tayari imeshatumwa kwa wahusika ambao sasa wanapaswa kuandaa utetezi wao haraka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala