Barcelona Apokea Kichapo Cha Mabao 3-1

0

Barcelona imekubali kipigo cha mabao 3-1 mbele ya Real madrid katika mchezo wa Laliga uliochezwa leo majira ya saa 10:00 jioni katika uwanja wao wa nyumbani wa Camp Nou.

Real Madrid walianza kupachika bao la kwanza dakika ya 5 kupitia Federico Valverde ambapo lilisawazishwa na Ansu Fati wa Barcelona dakika ya 8.

Bao la pili la Real Madrid lilipachikwa na Sergio Ramos dakika ya 63 huku dakika ya 90 kabla ya kipenga cha kumaliza mchezo kupulizwa Luka Modric alipachika bao la tatu la ushindi kwa klabu yake.

Real madrid wanabaki kileleni katika msimamo wa Laliga wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 13 kibindoni katika miichezo sita waliyocheza.

Leave A Reply

Your email address will not be published.