Connect with us

Makala

Bale Astaafu Rasmi Soka

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Tottenham na Real Madrid Gareth Bale amestaafu kucheza soka la ushindani rasmi kuanzia Jumatatu Januari 9 baada ya kutangaza taarifa hizo kupitia mitandao yake ya kijamii.

Staa huyo aliyeanzia soka katika vilabu vya Southampton kisha akaenda Tottenham ambapo alipanda thamani baada ya kuanza kutumika kama mshambuliaji wa pembeni badala ya beki wa kushoto na hatimaye kusajiliwa katika klabu ya Real Madrid ambapo alijiongezea umaarufu na utajiri mkubwa mpaka alipoamua kujiunga na Los Angels Fc ya nchini Marekani kabla ya kuamua kustaafu rasmi.

“Baada ya kufikiri kwa uangalifu ninatangaza kustaafu kucheza mpira haraka katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa”Ilisomeka taarifa hiyo ya kustaafu kwake.

“Ninajiskia mwenye bahati kufanikisha ndoto yangu ya kucheza mchezo niupendao ambao kwa kweli umenipa nyakati nzuri maishani mwangu kwa misimu 17 ya kuwa juu ambayo ni ngumu kujirudia licha ya ukurasa ujao kuniandalia mazuri zaidi”Alimalizia katika andiko lake hilo..

Hakufanikiwa kushinda mataji makubwa akiwa katika ligi kuu ya Uingereza mbai na tuzo binafsi mpaka pale alisajiliwa na Real Madrid mwaka 2013 kwa dau la rekodi ya dunia la paundi milioni 100 ambapo alisaini mkataba wa miaka sita akifanikiwa kuchukua mataji ya La liga mara tatu,Klabu bingwa barani ulaya mara tano na kombe la Copa De la Rey la nchini humo mpaka alipoondoka June mwaka jana kujiunga na Los Angels Fc ya nchini Marekani.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala