Connect with us

Makala

Aziz Ki Kutua Bongo Wiki Hii

Rasmi kiungo mshambuliaji raia wa Burkina faso Stephanie Aziz ki ameagwa leo na timu yake ya Asec Mimosas mara baada ya mchezo wa kumaliza msimu wa 2021-22 wa Ligi Kuu nchi Ivory Coast ambapo klabu hiyo imefanikiwa kutwa taji hilo.

Awali kabisa Yanga walipanga kumleta Stephanie Aziz ki nchini Jumatatu lakini Mambo hayakwenda sawa na Jana kupitia kwa Mkurugenzi wa uwekezaji Kutoka Gsm Eng Hersi Ally Said alithibitisha ujio wake akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole Ethiopia ambapo kiungo huyo atakuja kukamilisha baadhi ya vitu vichache kisha kusaini mkataba kamili wa kujiunga na klabu ya Yanga sc.

Stephanie Aziz ki ameanza safari usiku Kutoka Ivory Coast sambamba na wakala wake kuja nchini Tanzania na Leo majira ya usiku atakuwa nchini Tanzania na ataunganisha ndege moja kwa moja kwenda Arusha kushuhudia mchezo wa fainali dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Yanga sc itakua inacheza na Coastal union.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala