Connect with us

Makala

Azam Fc Yatolewa Muungano Cup

Azam Fc imesukumizwa nje ya michuano ya kombe la Muungano 2025 kufuatia kipigo cha 2-1 dhidi ya JKU FC ya Zanzibar kwenye nusu fainali katika mchezo uliofanyika katika Viwanja vya Gombani Visiwani Pemba.

Azam Fc iliyoanza na kikosi mchanganyiko na vijana pamoja na wale wanaoanzia benchi mara kwa mara ambapo Azam Fc walipata bao la kwanza dakika ya 15 ya mchezo likifungwa na Yeison Fuentes kwa shuti kali.

Kipindi cha pili Jku walisawazisha bao hilo kwa bao la kiufundi lililofungwa na Neva Adeline dakika ya 50 na kuufanya uwanja kujaa kwa furaha.

Jku ilipata bao la pili kupitia kwa Fred Sliman dakika ya 80 ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo huo.

Baada ya mpira kuisha mfungaji wa bao la pili la JKU Fc, Fred Sliman amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo na anachukua zawadi yake kutoka City Institute of Health, Dar es Salaam.

Jku Fc sasa baada ya ushindi huo imetinga fainali kumsubiri mshindi kati ya Zimamoto Fc dhidi ya Yanga sc watakaochuana Aprili 29 2025.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala