Home Soka Azam Fc Yamtema Amoah

Azam Fc Yamtema Amoah

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Azam Fc imetangaza kuachana na beki Daniel Amoah aliyedumu klabuni hapo kwa miaka nane tangu aliposajiliwa mwaka 2016 akitokea Medeama Fc ya nchini Ghana ambapo mchezaji huyo amekua nahidha wa Azam Fc kwa vipindi kadhaa.

Azam Fc imeamua kuachana na beki huyo ambaye mkataba wake umefikia ukingoni na kuamua kutomuongeza baada ya kuwa na uhakika na safu ya ulinzi iliyochini ya Yannick Bangala na Yeison Fuentes ambao wameunda safu kali na imara inayomvutia kocha Yousouph Dabo.

banner

Amoah amekua akitumika kama mbadala mara kadhaa akitokea benchi ama kutocheza kabisa huku akizidiwa na Edward Manyama kama mbadala ya Fuentes na Bangala na hivyo mara nyingi kujikuta anaishia jukwani ama benchi.

Azam Fc inaendelea na maboresho ya kikosi ikiwa tayari imewasajili viungo Ever Meza na mshambuliaji Jhonier Blanco aliyetokea nchini Colombia kuja kuongeza nguvu ya kikosi hicho ambacho msimu ujao kitashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited