Connect with us

Makala

Azam Fc Yamkomalia Ibenge

Klabu ya Azam Fc imeamua kukaza buti katika kuimendea saini ya kocha Frolent Ibenge kuja kuifundisha timu hiyo msimu ujao ili kuongeza maarifa zaidi baada ya kushindwa kufanya vizuri katika ligi kuu na michuano ya kimataifa msimu huu.

Kikosi hicho licha ya kusheheni mastaa mbalimbali wenye uwezo mkubwa imekua ikishindwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini ikiishia katika nafasi ya pili,tatu ama nne licha ya kuwa na miundombinu ya kisasa zaidi nchini.

Mpaka sasa klabu hiyo ipo katika nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu nchini ikiwa na alama 47 nyumba ya Yanga sc iliyo kileleni kwa alama 65 na Simba sc iliyokatika nafasi ya pili kwa alama 57 na Singida Big Stars yenye alama 48.

Mabosi wa juu wa klabu hiyo baada ya kuachana na kocha Dennis Lavigne mpaka sasa hawajaleta kocha mkuu huku kocha wa makipa Dani Cadena akisimama kama kocha mkuu licha ya kuwa na  leseni ya juu ya UEFA Pro ya Ukocha wa makipa.

Ibenge anatajwa kuja kuchukua nafasi hiyo ya ukocha mkuu wa klabu hiyo huku Cadena akirudishwa katika nafasi yake ya kocha wa makipa japo Azam Fc watakutana na ugumu wa kutosha kumng’oa kocha huyo kutokana na klabu yake ya sasa Al Hilal Ordourman kutokua tayari kumuachia kirahisi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala