Connect with us

Makala

Azam Fc ‘Out’ Mapinduzi Cup

Klabu ya soka ya Azam Fc imeungana na klabu za Simba sc na Yanga sc baada ya kutolewa katika michuano ya kombe la Mapinduzi kutokana na kukubali kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Singida Big Stars katika mchezo wa nusu fainali uliomalizika katika uwanja wa Amani mjini Unguja visiwani Zanzibar.

Timu zote mbili ziliingiza vikosi vyake vya kwanza vilivyosheheni mastaa wote ikiwemo waliosajiliwa hivi karibuni lakini Singida Big Stars ilianza kupata majibu ya ubora wa sajili zake baada ya Francy Kazadi kuandika bao la kwanza dakika ya 27 baada ya kipa kinda wa Azam Fc Zubeir Foba kufanya makosa.

Abdul Sopu alisawazisha dakika ya 43 ya mchezo baada ya kumalizia mpira uliomshinda beki wa Singida Big Stars na kuuweka wavuni lakini Kazadi alifunga tena mabao matatu zaidi dakika za 53,64 na 86 na kuumaliza kabisa mchezo huku mabao hayo yakichangiwa na uzembe wa safu ya ulinzi ya Azam Fc pamoja na makosa ya kujirudia rudia ya kipa Zubeiry Foba.

Singida Big Stars sasa inasubiri mshindi kati ya Namungo Fc na Mlandege ili kufahamu itacheza na nani mchezo wa fainali ya michuano hiyo maarufu visiwani humo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala