Connect with us

Soka

Ndayiragije,Samatta Watofautiana

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Ettiene Ndayiragije na nahodha wa kikosi hicho Mbwana Samatta wametofautiana katika kupiga kura ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanaume baada ya mmoja kupiga kura kwa wachezaji tofauti.

Kura hizo ambazo hupigwa na manahodha na kocha wa timu husika pamoja na waandishi wa habari walioidhinishwa zilionyesha kwamba kocha huyo aliwapigia kura Messi,Ronaldo na Mohamed Salah huku Samata akiwapigia Virgil Van Djik,Kylian Mbappe na SadioManne.

Mgawanyiko wa kura hizo unaonyesha jina la kwanza huwa na pointi 5 huku la pili likiwa na pointi 4 na la mwisho huwa na pointi 3 na mshindi ni atakaepata pointi nyingi baada ya kufanyiwa majumuisho.

Tuzo hizo zilihitimishwa jana ambapo Lionell Messi aliibuka kidedea akiwabwaga wapinzani wake Cristiano Ronaldo na Virgil van Djik.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka